LUPITA NYONGO AWACHEFUA KENYA SOMA KISAHIKI.
STAA huyo kutoka Hollywood mwenye asili ya Afrika mashariki zao la Kenya inchi karibu na Tanzania, alimaharufu kama Lupita Nyongo jina alilo pewa na wazazi wake, hivi
karibuni amejikuta akiwaboa ndugu zake Wakenya baada ya kushindwa kuhudhuria uzinduzi wa Filamu ya Black Panther uliofanyika nchini hapo Jumanne iliyopita.
Mashabiki wa mwanadada huyo kutoka Kenya, walianza kuonesha kutofurahishwa na suala hilo baada ya Lupita
Kuonekana kwenye uzinduzi wa filamu hiyo Afrika Kusini huku akiwa amekacha uzinduzi wa filamu hiyohiyo nchini Kenya.
Hata hivyo, pamoja na lawama na madongo ambayo mwanadada huyo ametupiwa na mashabiki wake juu ya kuwasusa ‘nduguze’, hakujibu lolote wala kueleza ni kwa nini alikosekana kwenye uzinduzi wa Black Panther Kenya.